Ndio, lugha, tunazo nyingi.
Neno zinge kuwa shillingi,
Tunge kuwa zote matajiri.
Tusi jilinganishe na mti,
Mwenye tuna muona kwa runinga,
Ati matawi zake na zangu za fanana rangi.
Jilinganishe na Jirani.
Mwenye ana eza kutunza watoto,
Tukienda kazi.
Siku ijayo, nikikosa.
Ndye atanisaidia chumvi.
Bega kwa bega,
Tunayo nguvu ya kuhakikisha uhai ya amani.
Tusikubali kuwa nyasi,
Ndovu zikipigania Udume.
Vijana tuungane, wewe na mimi,
Ili kesho tukule, leo, tulime.
Reblogged this on andikapoetry and commented:
a swahili piece by @Raya_Wambui enjoy..
Ubunifu sawa kabisa,shairi lina mtiririko sawa ingawaje umeruhusiwa,sharti utazame mpangilio wa shairi vyema kwa kuongazia (a)vina (b)ngeli na pia jaribu kutumia inkisari kuendeleza na kuonyesha ujuzi na ueledi wako kama mtunzi,kongole gwiji endelea na utunzi